USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya
Klabu ya Arsenal inakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 45 kumchukua kiungo wa AS Monaco, Thomas Lemar mwenye umri wa miaka 21. (Sun)
Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 45 kumchukua kiungo wa Monaco, Thomas Lemar
Monaco wamekataa dau la tatu la Arsenal la pauni milioni 44.7 la kumtaka, Thomas Lemar. (L’Equipe)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hawezi kutoa hakikisho kuwa, Gareth Bale atabakia Bernabeu msimu huu, huku Manchester United wakimfuatilia. (Mirror)
Mchezaji wa Real Madrid, Gareth Bale
Monaco watakuwa tayari kumuuza, Kylian Mbappe kwa timu itakayokuwa tayari kutoa euro milioni 180. (L’Equipe)
Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte anapanga kutoa pauni milioni 50 kuwasajili wachezaji, Ross Barkley mwenye umri wa miaka 23, kutoka Everton na Alex Oxlade-Chamberlain 23, kutoka Arsenal. (Sun)
Winga wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez
Chelsea wamepanda dau kutaka kumsajili kwa mkopo Renato Sanches, 19, kutoka Bayern Munich. (Daily Telegraph)
Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochetitino anataka kumsajili mchezaji, Ross Barkley na kumfanya kuwa kiungo wa kati huku Roma wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka winga wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez, anayechezea Leicester. (Mirror)
Liverpool wapo tayari kutoa dau la mwisho la zaidi ya pauni milioni 70 kujaribu kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22. (Mirror)
Liverpool wanashikilia msimamo wao kuwa Philippe Coutinho, 25, hauzwi, huku Barcelona wakiendelea kumfuatilia. (ESPN))
Limerpool- kwa shingo upande- wameweka bei ya Philippe Coutinho kuwa ni pauni milioni 133, kama kweli Barcelona wanamtaka mchezaji huyo kutoka Brazil. (Sport)
Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti amesema anataka Ivan Perisic kubakia Italia, ingawa hana uhakika kama ataweza kufanya hivyo huku Manchester United wakiendelea kumfuatilia. (ESPN) Sport)
Inter Milan wameweka kipaumbele katika kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, na wanajiandaa kutoa dau la euro milioni 50. (Gazzetta dello Sport)
Juventus wanaotafuta kiungo mkabaji sasa wamemgeukia Blaise Matuidi, 30, wa PSG, baada ya kuacha kumfuatilia Nemanja Matic, 28, anayenyatiwa na Manchester United. (Independent)
Mwenyekiti wa AC Milan Marco Fassone amesema klabu yake imezungumza na wakala wa mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzima, 29, anatarajiwa kusaini mkataba mpya hata kama klabu yake itamsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Marca)
Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Paulo Dybala, 23, anayenyatiwa na Manchester United na Barcelona, hana mipango ya kuondoka Juventus msimu huu. (TalkSport)
Wakala wa mchezaji wa Arsenal Lucas Perez amekwenda London kuzungumzia kurejea kwa mshambuliaji huyo Deoportivo La Coruna. (AS)
Neymar na mchezaji mwenzake wa Barcelona wazichapa mazoezini (+Video)
Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona, Neymar Jr leo asubuhi amejikuta akitengeneza vichwa vya habari duniani baada ya kupigana na kinda wa Barcelona, Nelson Semedo wakiwa mazoezini nchini Marekani.
Kwa mujibu wa Gazeti la Marca taarifa zinasema Neymar alichezewa rafu na Nelson Semedo aliyesajiliwa msimu huu kutoka Benfica kitu ambacho alikichukulia kama amefanyiwa makusudi na ndipo akaanza kuvutana na kuanza kurushiana makonde.
Kwenye video iliyotolewa na mtandao wa Daily Mail inaonesha Neymar akionekana mwenye hasira kwani licha ya kuamuliwa na Javier Mascherano aliendelea kumfuata Nelson ili wazichape.Hata hivyo ugomvi huo uliisha ingawaje Neymar alivua nguo za mazoezi na kurudi chumbani kwake huku akiwaacha wenzake wakifanya mazoezi.
Tayari kumeanza minong’ono kuwa kitendo hicho huenda kikawa kama chanzo cha yeye kuihama klabu hiyo baada ya tetesi za kuwindwa na matajiri wa ufaransa, PSG.
No comments:
Post a Comment