Kupitia instagram account ya 50 Cent alionyesha kukasirishwa na maneno ya shabiki huyo na kupost picha yake (Birightimuze) na kuandika caption “This guy just asked why i only show 1 son, because l only have a relation ship with 1, but why do he want to know? I don’t give a …… about them dirty ass kids on his page. #denofthievesAkimaanisha kuwa “Huyu kijana anauliza kwa nini naonyesha mtoto mmoja?? kwasababu nina mahusiano na mtu mmoja lakini kwa nini anataka kujua?? sijali kuhusu watoto wake wachafu kwenye page yake, Tafadhali kaa mbali na maisha yangu”
Idara ya afya ya Mashariki mwa Cape own nchini South Africa ilitoa onyo baada ya watu zaidi ya 50 ambao walikula nyama ya ng’ombe waliokufa kupelekwa hospitali mbalimbali Alhamisi katika jimbo hilo.
Wagonjwa hao walikuwa na dalili ikiwa ni pamoja na kuhara, kutapika, maumivu ya kichwa na ya tumbo. Wao walielezea kwamba walikuwa wamekula nyama ya ng’ombe aliyekufa baada ya kuumwa na nyoka
Wema Sepetu kuja kivingine, Juni 30
Malkia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu baada ya kufungua App yake sasa anakuja na kitu kingine ambacho bado kipo kwenye mabano hadi ifikapo Juni 30, 2018.
Muigizaji huyo amekuwa aliwaomba mashabiki wake kuitunza tarehe hiyo na kuikumbuka ili kufahamu kiundani ujio wa siku hiyo
Ujumbe huo ametuma Kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Diamond Platinumz aendelea kudhirisha ushikaji wake na mlimbwende Wema Sepetu kwa kumsapoti katika hili kwa kuposti kwenye ukurasa wake na kuandika ”Save the date” huku Wema akimjibu You are the Best”.
Ni kweli bado haijawekwa wazi nini hasa kina kuja, kwani tunavyojua Wema Sepetu ni mwanamke aliyejikita katika shughuli mbalimbali katika jamii.
Hivyo kaa tayari.
Kupitia ukurasa wake wa Instagrama Wema Sepetu ameandika,
Just save the date,
wiki,week 21
siku/day 151
A BOY FROM TANDALE
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesogeza mbele tarehe ya kuachia album yake ya kwanza ya ‘A Boy From Tandale’.Album hiyo ambayo awali ilitangazwa kuachiwa tarehe 23 Februari mwaka huu imesogezwa mbele hadi tarehe 7 Machi 2018.
Uongozi umeeleza kuwa sababu kubwa ya kusogeza tarehe mbele ni kupisha zoezi la utambulisho na kusimamia kazi za msanii mpya wa WCB, Mbosso ambaye ametambulishwa wikiendi iliyopita.
Tazama Mbosso alivyotambulishwa na Diamond Platnumz ‘WCB’.
VIDEO ON TWITTER
Mwanamasumbwi nchini Marekani, Floyd Mayweather ameamua kulifanyia kazi wazo lake la kuingia katika mapambano ya karate ‘mixed martial arts’ mchezo ambao hutumia viungo vyote vya mwili badala ya kutumia mikono pekee.
Mayweather amelithibitisha hilo baada ya hapo jana siku ya Jumanne kuposti picha zake na kipande cha video kinachomuonyesha akiingia katika ulingo wa mchezo huoKiongozi huyo wa timu ya The Money aliposti kipande hicho cha video bila kuandika kitu chochote ikiwa ni kama ishara ya kuingia katika mchhezo huo.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 40 alirejea katika mchezo wa masumbwi baada ya kupigana na McGregor na kushinda katika pambano lake la 50 pasipo kupoteza hata moja
WCB ni chama la wana – Diamond
Msanii wa Bongo Flava na Mmiliki wa Label ya WCB, Diamond Platnumz amesema label hiyo ni kwa ajili ya msanii yeyote yule, hivyo ni mapema kusitisha zoezi la kuchukua wasanii wengine hasa wale wanaochipukia
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Eneka’, ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa WCB itaendelea kuchukua wasanii wapya ila itatengemea zaidi support watakayozidi kupata kutoka kwenye vyombo vya habari.
“Unajua sisi tunasemaga WCB ni chama la wana kwa sababu sisi tunajaribu kuchukua watu wa aina tofauti tofauti kutoka kwenye mtaa na mimi siwezi kuwasaidia pekee yangu ndio maana namleta kwenye media ili afikie malengo yake na watu wengi wapo mitaani wanaohitaji msaada,” amesema Diamond na kuongeza.
“Kwa hiyo tukisema tunaaacha ina maana unakatisha ndoto za vijana wengi ambao wanaamini wanaweza kuwa ndani ya WCB, lakini support tutakayopata ndio itasema tuendelee kusainisha watu au tusitishe, kama support hamna mimi mwenyewe Diamond Platinumz nitaachia mangoma yangu,” amesisitiza.
WCB hadi sasa ina wasanii sita ambao Harmonize, Rich Mavoko, Queen Darleen, Rayvanny, Lava Lava na Diamond mwenyewe.
JAMANI MIMI NA MPENDA SANA HUYU MTOTO BEKA FLAVOUR ASEMA RAY C
Muimbaji Rehema Charamila aka Ray C ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Unanimaliza’ amefunguka na kusema yeye anampenda sana msanii kutoka kundi la Yamoto Band, Beka Flavour na kusema anaamini atafika mbali sana.
Ray C alisema anaposikiliza wimbo wake ‘Libebe’ anapata kusikia muziki wa bongo fleva halisi kabisaa ambayo ilikuwa inafanywa na wasanii wakubwa miaka ya nyuma.
“Jamani mimi nampenda sana huyu mtoto Beka Flavour, kila nikisikiliza wimbo wake ule ‘Libebe’ namuona mbali sana kwani kazi yake ni nzuri sana yule kijana, hakika akipata usimamizi mzuri atafika mbali mno, maana anaimba ile bongo fleva halisi kabisaa” alisema Ray C
Beka Flavour ni msanii kutoka kundi la Yamoto Band ambaye amekuwa msanii wa pili kutoka katika kundi hilo kuachia kazi ya peke yake na kupokelewa vizuri naWatanzani, hata hivyo Beka Flavour ameahidi kuwa ataendelea kuleta kazi nzuri na hawezi kuwaangusha Watanzania.
Kuna ‘vichupi kunuka’ wanajifanya wanajua sana – Diamond
Diamond Platnumz ameamua kuwaumbua waliokuwa wakisema kwamba penzi lake za Zari limekufa.
Pia amewajibu wanaotaka mpenzi wake abaki akiwa mnyonge baada ya kupata matatizo ya kufiwa na mama yake mzazi wiki chache zilizopita.
“Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa Misiba ya watu…. Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehem tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja!…sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia… Pambaneni na Mahusiano yenu…! Nina siku 5 za kumpetipeti… leo ndio kwanza Ya kwanza 😛.” ameandika Diamond Instagram.
Diamond amefikia hatua hiyo baada ya watu kumponda mpenzi wake Zari The Boss Lady, ambaye siku ya jana alikuwa Instalive na mkali huyo wa Eneka wakijiachi kimahaba, hali iliyofanya mitandao ya kijamii kumponda kuwa anaonyesha hana uchungu wa kufiwa na mzazi wake, kazi yake ni kujiendekeza na mapenzi.
Picha zilizozua mijadala mitandaoni.
No comments:
Post a Comment